Wananchi wa Mkoa wa Manyara hasa jamii za kifugaji wametakiwa kuacha kuharibu Miundombinu ya maji inayotekelezwa kwa gharama kubwa na Serikali ambapo baadhi Yao wemekuwa wakitumia Mikuki kupasua mabomba ya Maji kwaajili ya matumizi yao ikiwemo kunyweshea mifugo.
Agizo hilo limetolewa na katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo wakati akikagua Mradi wa Maji Mogitu-Gehandu ambao mpaka kukamilika kwake utagharimu Shilingi Bilion 5 lenye uwezo wa kuhidhi Maji Lita Milioni moja huku akipongeza jitihada zinazofanywa na RUWASA mkoa wa Manyara.
Chongolo amesema ameridhishwa na hatua zinazochukuliwa na RUWASA mkoa wa Manyara katika kuhakikisha wanatekeleza adhma ya Rais Samia ya kumtua Mama ndoo kichwani na maji kupatikana katika maeneo yote.
Nae Meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara Mhandisi Wolta Kirita Mradi huo ukikamilika utakwenda kusadia kukuza uchumi wa wananchi wa maeneo hayo kwani walikuwa wakitumia muda mwingi Kutafuta Maji hivyo Sasa watatumia muda huo katika shughuli nyingine za Maendeleo baada ya kuwa na maji katika maeneo yao.