Ni Julai 28, 2023 ambapo Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Silaa anazungumza muda huu kupitia kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa Clouds FM 88.5.
“Wanaosema bandari inauzwa, waonyeshe watu mahali panaposema mauziano, kwa sababu hata ibara ya 12 (1) inaongelea mambo ya ulinzi katika mkataba huu wa uwekezaji wa bandari na wala sio kuuziana kama watu wanavyojaribu kusema” – Jerry Silaa Mbunge Ukonga.
“Watanzania wote wana haki ya kuzungumzia mkataba huu, lakini lazima tuuweke kisheria. Bahati mbaya katika wapotoshaji hawa wakati mwingine hawatumii hoja za msingi jambo linalopoteza maana ya majadiliano mitaani,” Jerry Silaa Mbunge Ukonga.
“Wawekezaji wengi walileta maombi yao ili wapate haki ya kuendesha bandari yetu, lakini watu wa bandari wao wanajua ni watu gani wanawahitaji kwa kuangalia vigezo na mahitaji. Makampuni yaliyoleta maombi ni Hutchson (Hong Kong), Antewerp/Brugge (Belgium), PSA International (Singapore), DP World (Dubai), Abu Dhabi Ports (Abu Dhabi), Adani Ports and Logistics (Mundra-India), Kampuni ya CMA-CGM (France) pamoja na Kampuni ya Maersk (Denmark),” Jerry Silaa Mbunge Ukonga