Mataifa ya Kenya, Djibouti, Madagascar na Mauritius yamewasilisha rasimi majina ya watu wanaopendekezwa kuwania uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika AUC.
Nchi wanachama 55 kutoka mataifa wanachama wa AU zinatarajiwa kukutana katika kongamano la mwezi Februari mwaka ujao kumchagua mrithi wa mwenyekiti wa sasa Moussa Faki Mahamat.
Mwaka huu, nchi wanachama wa EAC zimepwa nafasi ya kutoa mrithi wa Faki, raia wa Chad ambaye amehudumu tangu mwaka wa 2017.
Umoja wa Afrika umechapisha majina ya watu wanne wanaowania nafasi hiyo akiwemo Mahamoud Ali Youssouf kutoka Djibouti, Raila Odinga wa Kenya, Richard Randriamandrato wa Madagascar na Anil Gayan raia wa Mauritius.
“Mimi ndiye mgombea peke ninayeweza kuzileta pamoja nchi za Afrika zikiwemo zile zinazozungumza Kifaransa, Kiingereza au Kiarabu.” alisema Youssouf raia wa Djibouti.
Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 58 amekuwa waziri wa mambo ya kigeno katika taifa hilo dogo la pembe ya Afrika tangu mwaka wa 2005.
“Iwapo nitachaguliwa, lengo langu ni kunyamazisha milio ya risasi katika bara la Afrika.” alieleza katika mahojiano na AFP mwezi uliopita.