Kulingana na ripoti ya Daily Mail, wanaume wengi nchini Marekani pia wamekuwa wakijaribu kufikia mwili wa utanashati na muonekano mzuri kwa msaada wa upasuaji wa urembo.(plastic surgery)
Takwimu kutoka kwenye Jumuiya ya Madaktari wa Upasuaji wa Plastiki ya Marekani zinaonyesha kuwa wanaume milioni 1.3 nchini Marekani wamekuwa wakitumia madaktari wa upasuaji wa kutengeneza mionekano kila mwaka ikiwa ni taratibu za urembo, kutengeneza pua, kifua na wengine kutengeneza makalio kwa vifaa maalum na maarufu vya Brazili.
Dk. Jones alibainisha kuwa wanaume wengi pia wanapata surgery wa mwili ili kupata mwili wenye muonekano bora zaidi. “Ninaona kwamba wanaume wanataka sana hilo lifanyike ili waweze kuonekana wenye misuli zaidi.”
Aliendelea, “Wagonjwa wangu wanaopata BBLs Ninapata wakufunzi wengi wa gym ambao wana maeneo fulani wanataka kushughulikia.
Pia nina wagonjwa wakubwa wa kupunguza uzito ambao wana ngozi iliyozidi (unene)na wameitunza.
Nina maafisa wa polisi waliostaafu na watoto wa chuo kikuu. Ni wigo mpana sana, “alisema kwenye kituo hicho.