Katika kuelekea siku ya kifua kikuu duniani ambayo huazimishwa machi 24 kila mwaka shirika la mwitikio wa kudhibiti kifua kikuu na ukimwi tanzania {MKUTA } limetoa elimu kwa waandishi wa habari juu ya uelewa wa maambukizi na namna ya kupambana na kifua kikuu nchini Tanzania.
Moja ya malengo ya taasisi hii ni kushiriki katika wiki hii kuwatafuta na kuibua wagonjwa ndani ya wilaya mbalimbali nchi na kuwasaidia kupata matibabu na elimu juu ya kifua kikuu kama moja ya malengo ya kutokomeza TB nchini ifikapo mwaka 2035 na kuadhimisha siku ya TB duniani kwa mwaka 2024 kukiwa na mabadiliko makubwa ya ufikiaji wagonjwa nchini.
Dokta Willy Mbelwa amesema kuwa nchi ya Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwa kipinda cha mwaka 2015 hadi sasa , na hii imetokana na juhudi za taasisi kuibua wagojwa na mchango wa jamii katika elimu juu ya tb huku serikali pamoja na wadau wakisaidia katika kuongeza dawa,ununuzi wa mashine za kisasa ,vifaa vya ufundishaji na upimaji wa tb na ujenzi wa vituo vya afya nchini.
‘Kwa miaka 5 iliopita mikoa ya Dar es laam ,Pwani ,Manyara,Arusha ,Njombe,imekuwa na uibuaji wa wagojwa wa TB huku Kigoma,Songwe,Simiyu ,Katavi, Kagera,na Visiwa vya Zanzibar ina kiwango cha chini cha uibuaji wa wagojwa’. Dkt Mbawala
‘Dkt. Mbawala maesema kuwa nchini Tanzania TB hugharimu wastani wa asilimia 7 ya pato la taifa,na kila mwaka watu 137,000 huugua na kusababisha vifo 32,000 sawa na vifo 87 kila siku ikichangiwa na gharama za matibabu na kukatisha dozi ya TB.
Zaidi ya watu Billioni 2 sawa na asilimia 25 wanaishi na maambukizi ya ugojwa wa kifua kikuu nchini hivi sasa huku makundi hatarishi ya kupata maambukizi yakiwa ni watu wenye magojwa sugu,wavuta sigara ,watu wanaoishi kwenye mazingira duni ,wanaoishi na wenye maambukizi ,wazee,wakimbizi nk.
Takwimu za wizara zinaonesha kuwa wanaume wengia huugua kifua kikuu kuliko wanawake wakiwa na hatari kubwa ya kufariki kwa ugojwa huu wa kifua kikuu.