Wanawake wametajwa kuwa waathirika wakubwa wa masuala ya migogoro ya ardhi hasa vijijini kutokana na kushindwa kupata msaada wa kisheria mapema na kupelekea kupoteza haki zao.
Hayo yamebainishwa na Afisa Tawala Wilaya ya Morogoro Hilari Sagara wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalim yaliyoandaliwa na Tasisi isiyo ya kiserikali ya Liberty Sparks na kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wasaidizi wa msaada wa kisheria (Paralegal Centre )kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa Morogoro ili kuwajengea uwezo kusadia jamii katika maeneo yao.
Sagara amesema Pamoja na kasi ya mabadiliko ya masuala ya usawa kwenye Nyanja mbalimbali katika jamii, imeelezwa kuwa bado wanawake wanakabiliwa na changamoto ya umiliki ardhi hasa vijijini, licha ya wao kuwa sehemu ya kuchagiza ukuaji wa uchumi wa Nchi na ustawi wa familia.
Aidha Sagara ametoa wito kwa taasisi za kisheria kufanya utafiti kujua kwanini Morogoro imekithiri changamoto ya migogoro ya ardhi huku kadiri siku zinavyokwenda inaongezeka kwa wingi.
Amesema anatambua jitihada zinazofanywa na taasisi za kisheria ikiwemo Paralegal Centre,TLS, Liberty Spaks na taasisi zingine kwa kuwasaida wananchi kupata haki zao hivyo wanawajibu kujua kwanini changamoto hiyo imekua kibwa wilaya ya Morogoro.
“Kila siku asubuhi ukija ofisi ya Mkuu wa Wilaya utakuta wananchi wamefurika waliowengi wanachangamoto ya migogoro ya ardhi na tumekua tukiwaelekeza waje kwenu wale wanaohitaji tafsiri za kisheria hivyo mnafanya jambo nzuri sana lakini ni vizuri mkachunguza nini chanzo cha migogoro hii”
Anasema wanawake waishio vijijini hushuhudiwa wakiwa sehemu ya uzalishaji katika sekta ya kilimo, lakini suala la umiliki wa ardhi limeendelea kuwa kitendawili kwao, uelewa mdogo wa masuala ya kisheria ya umiliki ardhi ukionekana kuwadidimiza.
Mkurugenzi wa Taaisisi ya Liberty Sparks Evans Exaud anasema kuna haja ya kuona umuhimu wa kutengeneza mazingira rafiki ya kisera zenye kufungua uelewa wa utambuzi wa misingi ya umiliki ardhi kwa kupanua wigo katika utoaji wa hatimiliki.
Anasema kutokana na changamoto hiyo imewasukuma kuwakutanisha wadau mbalimbali lengo kuendelea kusaidia kutatua Migogoro ya ardhi hasa kwa wanawake wajane ambao wamekua waathirika wakubwa pindi wanapofika na wanaume zao.
Kwa upande wake Peter Kimath- Kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria Paralegal Centre anasema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali lakini wameendelea kusaidia wananchi katika masuala ya utambuzi wa masuala ya kisheria wakiwemo wanawake kutambua haki ya kumili ardhi.
Anasema kituo hicho kimeweka wasaidizi maeneo mbalimbali ya mkoa wa Morogoro hivyo lengo kuweka wanaseheria katika maeneo hayo ili kuendelea kusaidia jamii hasa wenye uchumi mdogo.
Anna Alex ni mkazi wa Morogoro kutoka jamii ya wamaasai, anasema iko haja ya jamii kutowabagua wanawake katika masuala ya umiliki ardhi, kilio chake akikipeleka kwa wanawake wajane namna wanavyokandamizwa kupata haki zao stahiki
Anasema bado wanawake hasa jamii ya kimasai inahitaji elimu zaidi ya kutambua haki zao katika umiliki wa mali kwani jamii hiyo bado ipo nyuma kielimu na kuziomba taasisi mbalimali kuendelea kusaidia kundi hilo.