Watafiti kutoka kituo cha utafiti wa usingizi cha Chuo Kikuu cha Loughborough Nchini Uingereza wamesema Wanawake wanahitaji muda mwingi zaidi wa kupata usingizi kwasababu wanatumia zaidi akili zao kuliko Wanaume.
Profesa Jim Horne kutoka Chuo hicho amenukuliwa akisema “akili za Wanawake zimeunganishwa kwa njia tofauti hivyo hitaji lao la kulala litakuwa kubwa zaidi, Wanawake huwa na kazi nyingi kuliko Wanaume, hufanya maamuzi mara moja na wanaweza kubadilika hivyo hutumia zaidi ubongo wao halisi kuliko Wanaume lakini hata homoni zao zinaweza kuwa sababu nyingine ya kutofautiana kwa mahitaji ya usingizi kati ya Mwanaume na Mwanamke”
Amesema mzunguko wa kulala kwa Wanawake unatawaliwa na homoni na kwamba homoni hizi huathiri Wanawake na kuhisi uchovu na wakati mwingine wanahisi njaa ambapo pamoja na kwamba utafiti unaonesha Wanawake wanahitaji kulala zaidi kuliko Wanaume lakini pia tafiti zinaonesha Wanawake huwa na usingizi mrefu kidogo kuliko Wanaume, wakilala kwa zaidi ya dakika 11 mbele ya Wanaume.