Katika muendelezo wa matukio ya visa vipya vya maambukizi ya Virusi vya Corona, hali imefikia pabaya hadi hatua ya wanyama kama Paka,Chui, Simba na Mbwa kupata maambukizi ya ugonjwa huo.
Katika taarifa mpya iliyotolewa na mtandao wa TMZ nchini Marekani, inathibitisha kuwa kumekuwa na maambukizi ya kwanza kwa wanyama aina ya Paka kupata virusi vya ugonjwa huo.
Wataalamu wa wanyama nchini humo wamesema virusi hivyo wamevipata kutoka kwa binadamu ila wanategemea watapona ugonjwa huo.
Aidha kupitia ripoti ya ABC, inaeleza kuwa wanyama wengine saba ambao ni Chui aina ya Tiger, na Simba watatu wamekutwa na Virusi vya ugonjwa wa Corona katika Zoo ya Bronx jijini New York nchini Marekani.
Siku kadhaa zilizopita Zoo hiyo ilitangaza kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Corona kwa Tiger mwenye miaka minne anayejulikana kwa jina la Nadia.
Ikumbukwe tu hata jijini Hong Kong nchini China, tayari wameshatangaza visa vya virusi hivyo vya Corona kwenda kwa wanyama aina ya Mbwa ambavyo sababu yake imetokea kwa binadamu.