Raia wa Liberia, wanatarajia kurejea tena kwenye sanduku la kura Jumanne ya wiki ijayo, kuchagua kati ya rais George Weah au makamu wa rais wa zamani, Joseph Boakai, baada ya duru ya kwanza wagombea hawa kutofikisha asilimia 50 ya kura zote.
Baada ya matokeo ya duru ya kwanza, George Weah alipata asilimia 43.83 ya kura zote huku mpinzani wake Joseph Boakai, yeyé akipata asilimia 43.44 ya kura zote na kuwalazimisha kwenda kwenye duru ya pili.
Tofauti ndogo ya kura walizopata kwenye duru ya kwanza na kutoshiriki kwa mgombea aliyeshika nafasi ya tatu kwenye uchaguzi huo, kunamaanisha kuwa uchaguzi wa wiki ijayo utakuwa wa ushindani mkubwa.
Uchaguzi wa Jumanne ijayo ni kama marudio ya ilivyokuwa mwaka 2017, ambapo baada ya duru ya pili, Weah alimshinda Boakai kwa kupata ushindi wa asilimia 61.54, wengi wa waliomchagua waki wa Vijana ingawa safari hii wameonesha kutokuwa na Imani nae tena.