Mamlaka nchini Chad ilisema Machi 24 iliwazuia wagombea 10, wakiwemo wapinzani wawili wakali wa utawala wa kijeshi, kugombea katika uchaguzi wa rais tarehe 6 Mei.
Mahakama ya kikatiba ilisema maombi ya wagombea hao – yaani yale ya wapinzani wakubwa Nassour Ibrahim Neguy Koursami na Rakhis Ahmat Saleh – yamekataliwa kwa sababu yalijumuisha “makosa”.
Wagombea wengine kumi wamesalia kwenye kinyang’anyiro hicho – maarufu zaidi kiongozi wa sasa wa junta Mahamat Idriss Deby Itno na waziri mkuu wake Succes Masra.
Jenerali Deby Itno alitangazwa rais na junta ya majenerali 15 mnamo 2021 kufuatia kifo cha babake Idriss Deby Itno, ambaye alitawala nchi ya Sahel kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miongo mitatu.
Rais huyo mpya aliahidi kurudisha madaraka kwa serikali ya kiraia ndani ya miezi 18 na kuuambia Umoja wa Afrika kuwa hatagombea kuchaguliwa kuwa rais.