Aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Jack Warner amengia kwenye headlines kwa mara nyingine tena September 29. Jack Warner ambaye alistaafu nafasi hiyo miaka minne iliopita, kamati ya maadili imetangaza kumfungia maisha kutojihusisha na masuala ya soka.
Jack Warner alikuwa akituhumiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo kula rushwa katika mchakato wa kuchagua nchi gani itaandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na mwaka 2022. Mchakato ambao unaaminika kuwa ulitawaliwa na rushwa na haukuwa wa haki.
Makamu huyo wa zamani wa Rais wa FIFA mwenye umri wa miaka 72 alikuwa ni moja kati ya maafisa wa FIFA waliotajwa mwaka huu kwa makosa ya rushwa, kutakatisha fedha haramu ikiwemo kufanya ulanguzi pamoja na kufanya udanganyifu wa pound milioni 100.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE