Wasanii wa nyimbo mbalimbali mkoani Morogoro wamesema changamoto kubwa inayowakabili ni kukosa mitaji na wafadhiri ambao wanaweza kuwaunga mkono Ili waweze kufanikiwa.
Wakizungumza na Ayo tv baadhi ya wasanii hao wakati WA Uzinduzi WA albam ya msanij Duzu wa mkoani Morogoro ,wamesema Morogoro kuna vipaji vingi lakini kinachokosekana ni ushirikishwa.
Amina kidevu ni mmoja wa wasanii nyimbo za taarabu anasema licha ya kukosa wafadhiri lakini hata Serikali mkoani humo haiwapi kipaumbele kwa kuwasaidia hasa Kwenye matamasha mbalimbali kama maeneo mengine
Anasema Ili msanii afahamike anatakiwa aanze nyumbani Kwake kukubalika hivyo kuimba Kwenye matamasha mbalimbali kunawapa utambulisho na kuamini na watu wengine.
Kwa Upande wake Msanii Duzu ambaye amezindua albamu yenye nyimbo 20 amesema licha ya kuanza kuimba muda mrefu lakini bado anashindwa kumudu gharama za kurekodi nyimbo hizo .
Anasema amekaa kwa kipindi kirefu nila kuimba hadi alipopata mfadhiri hivyo suala ka mitaji ni changamoto inayowakabali wasanii wengine Morogoro.
Johh Mselu mkazi wa Morogoro amesema Sasa ni wakati sahihi Kwa wasanii na watu wengine maarufu Morogoro kumtumia umaarudu kunufaika.
Anasema kipindi Cha nyuma mkoa huo ulikua na watu wengi maarufu lakini kwa sasa wanaishi maisha ya ombao omba hivyo wanatakiwa kuniwekeza pindi wanapopata fursa za kupata fedha .