Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitiza Wadau wa Utamaduni na Sanaa wakiwemo Wasanii ambao wamenufaika na ambao watanufaika na mikopo inayotolewa na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa kurejesha mikopo hiyo kulingana na makubaliano.
Pindi Chana ametoa agizo hilo leo February 23, 2023 alipofanya ziara katika ofisi za mfuko huo tangu ateuliwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia kuongoza Wizara hiyo.
“Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia fedha kwa ajili ya mfuko huu ambao una lengo la kusaidia Wadau wetu, nitoe rai kwenu Wadau kutumia fedha hizo kwa ajili ya kazi zinazokusudiwa ili muendeleze kazi zenu”
Amewataka Wadau wa Sanaa na Utamaduni kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo mikopo ya Halmashauri ili kuboresha kazi zao pia amemuagiza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Nyakaho Mahemba kuongeza uwezo wa kutafuta fedha kwa kushirikiana na Tasisi nyingine za fedha ili Wasanii wengi zaidi waweze kunufaika.