Ni Usiku wa Kuamkia Julai 22, 2023 ambapo Serikali ya Tanzania kupitia COSOTA imegawa pesa za mirabaha kwa Wasaniii ikiwa ni malipo yanayotokana na muziki wao kuchezwa maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye Radio na TV ambapo Msanii Diamond Platnumz ameongoza kwa kupata Tsh. milioni 7.7 akifuatiwa na Alikiba aliyepata Tsh. mil 5 .
Mirabaha hiyo imetolewa mbele ya Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Pindi Chana na Naibu Waziri wake Hamisi Mwinjuma maarufu @mwanafa .
Wengine waliopata mirabaha ni Rayvanny milioni 4.9, Mbosso milioni 4.9, Harmonize milioni 3.4, Zuchu milioni 4.9, Nandy milioni 3, Maua Sama milioni 2.3, Young Lunya milioni 1.6, Gnako milioni 1.3, Christina Shusho milioni 1.6, Rose Muhando mlioni 1 na Goodluck Gozbert milioni 2.1.