Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya mashariki ISaria Malisa amewataka wadau wa michezo hasa wa muziki na filamu kuhakikisha wanatumia maandhari zinazoleta uhalisia katika kazi zao Kwa kutumia hifadhi za Taifa zilizopo badala ya kutumia picha za mitandaoni.
Kamanda Malisa ameyasema hayo wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu fursa zilizopo katika Hifadhi za Taifa Kanda ya mashariki ikiwemo Mikumi,Udzungwa ,Saadani na Mwalimu Nyerere ambapo amesema bado baadhi ya wasanii wanashindwa kutumia hifadhi zetu kwa kuboresha kazi zao badala yake wanalazimika kwenda nchi za jirani kukamilisha maudhui yao.
Anasema kuna haja ya wasanii kuonesha mfano kwa Jamii hasa kuhamasisha masuala mbalimbali ambayo yamekua yanaleta tija kwa taifa Ili kuwa mfano bora Kwa jamii kwa kuitangaza nchi ya tanzania kupitika Utalii.
“Hapa nilipo nyuma yangu kuna Mnyama Tembo hivyo nikiimba nyinbo nikitaja Tembo maana yake mtu anamuona Tembo Kwa nyuma hii inaleta uhalisia na ndo ubunifu wa kazi”
Kwa upande wake Msanii mkongwe wa muziki nchini ambaye ni mdau wa Utalii Afande Sele amesema wazo la Wahifadhi ni nzuri hivyo milango iko wazi kwa wadau wa Sanaa katika kuboresha kazi zao hivyo wanaweza kutembelea hifadhi ya Mikumi ili kurekodi maudhui yao.
Anasema kwa karne hii hakuna haja ya wasanii kusafiri maeneo mbalimbali kufanya kazi zao badala ya kutumia fursa zilizopo wakati tayari Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan ameshaweka mazingira rafiki katika kuhamasisha Utalii.
“hapa hifadhi ya mikumi Kuna Viwanja vingi vya michezo unaweza kuandaa bonanza la michezo lifanyike hapa na ukapatiwa kibali baada ya kufuata Utaratibu”