Waandaaji wa tuzo za Grammy watoa tangazo rasmi na wamethibitisha wasanii watakaotumbuiza katika toleo la 66 la Tuzo hizo zinazopangwa kufanyika Februari 2024.
Awali Chuo cha Kurekodi kilikuwa kimethibitisha mwenyeji wa Tuzo za Grammy 2024, tangazo la wasanii watakaotumbuiza katika kile kinachoainishwa kuwa usiku mkubwa zaidi wa muziki, limeteka hisia za mashabiki kote ulimwenguni.
Chuo cha Kurekodi katika tangazo rasmi mnamo Desemba 2023, kilithibitisha kwamba toleo la 66 la Tuzo za Grammy litasimamiwa na mcheshi wa Afrika Kusini na mtangazaji wa TV Trevor Noah.
Hili litakuwa toleo la tatu mfululizo la Grammys Trevor Noah atapewa jukumu la kusimamia hadi sasa.
Tangazo la wasanii watakaotumbuiza kwenye Tuzo za Grammy 2024 zilizopangwa kufanyika Februari, lilianza Jumatatu, Januari 15, 2024, huku tangazo la awali likiwa na majina matatu pekee.
1.Dua Lipa
2.Billie Eilish
3.Olivia Rodrigo