Wasenegal wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo unaofuatia miaka kadhaa ya machafuko na mzozo wa kisiasa, huku upinzani na muungano unaotawala wakiwa na imani ya kushinda.
Yeyote atakayeibuka juu atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal, inayotazamwa kama kinara wa demokrasia katika mapinduzi ya Afrika Magharibi, kutoka kwa matatizo yake ya hivi karibuni na kusimamia mapato kutoka kwa hifadhi ya mafuta na gesi ambayo yanakaribia kuanza uzalishaji.
Hali ya sintofahamu ilitawala kuhusu matokeo ya kura ya Jumapili, huku matokeo rasmi hayakutarajiwa kabla ya mwisho wa juma na idadi kamili inahitajika ili kupata ushindi katika raundi ya kwanza.
Rais anayeondoka Macky Sall alikuwa ameonya dhidi ya kujitangazia ushindi mapema.