Leo October 4, 2016 Naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Wiliam Ole Nasha ameongoza wananchi wa Arusha kwenye misa ya kuaga mwili wa marehemu Theresia Alex Nguma katika kanisa la mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha.
Theresia Alex ni mmoja watafiti waliouawa na wananchi wa kijiji cha Ilinga mkoani Dodoma baada ya kudhaniwa ni wanyonya damu. Akizungumza kanisani hapo Waziri Ole Nasha amesema bado serikali inaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Imeelezwa Mpaka kufikia sasa jumla ya watu 45 wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma baada ya kuhusishwa na tukio kuwauwa kwa mapanga kisha kuwachoma moto watafiti wawili na dereva wa chuo cha utafiti wa udongo na maendeleo ya ardhi cha Seliani Arusha August 1 mwaka huu.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro pia ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kuchukua sheria mkononi bila badala ya kufikisha kwenye vyombo vya dola.
ULIPITWA NA KAULI YA KAMA SIRRO KWA WAHALIFU WA BUGURUNI? ITAZAME HAPA