Watanzania 9 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 9 ikiwemo kuiba mbolea yenye thamani ya Sh.Mil.16.9.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Bashir Mfinanga (61), Siliak Mwaipopo (50), Juma Waziri (34), Juma Salehe (29), Zakaria Ndaya (40), Abas Sikanvika (34), God Mshana (30), Masumbuko Fumbo (43) na Zephania Kigola (33).
Washitakiwa hao kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Neema Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Yusto Ruboroga.
Mashitaka Makuu katika kesi hiyo ya jinai namba 15 ya mwaka 2021 ni kuiba Mali iliyokuwa inasafirishwa pamoja na kukutwa na Mbolea iliyopatikana isivyo halali. Katika mashitaka hayo inadaiwa kosa la kwanza hadi la tano liliwahusu washitakiwa Mfinanga, Mwaipopo, Waziri, Salehe na Ndaya.