Wakati Serikali ikitarajia kuanza kwa safari treni ya Mwendokasi kupitia Reli ya SGR Watanzania wametakiwa kuajiandaa kuanza kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi mara baada ya Treni ya Kisasa itakapo anza kufanya kazi Kwa kuanzisha shughuli za biashara na Kilimo
Wito huo umetolewa na Kaimu Mwenyekiti kamati ya kudumu ya Bunge uwekezaji na mitaji ya Umma( PLC) Mhe. Agustine Vuma wakati wa ziara ya wajumbe wa Kamati hiyo ya kukagua miundombinu ya njia ya kusafirisha umeme katika Reli ya Kisasa (SGR), tarehe 18 Desemba, 2023 mkoani Morogoro.
Vuma amesema Watanzania wanatakiwa kuanza kujiandaa kutumia fursa za kiuchumi ikiwemo kusafirisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mazao pia wao wenyewe kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa kuwa Serikali imetumia Mabilioni ya fedha kuhakikisha mradi huo unatekelezeka na kukamilika kwa wakati
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ziara hiyo ni maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko ya kutaka Waheshimiwa Wabunge watembelee miradi hiyo kwa lengo la kuona, kukagua na kutoa ushauri kwa wizara husika juu ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa imamaslahi makubwa kwa Taifa.
Naibu Waziri Kapinga amesema dhamana waliopewa ni kusimamia mradi huo kwa kushirikia Shirika la Reli nchini (TRC), hivyo wanafanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa, kuhakikisha fedha zinatolewa na Serikali zinatekeleza miradi hiyo kwa wakati ili kufanikisha kuanza kutumika kwa treni hiyo ya kisasa ambayo ni moja ya maeneo yatakayoleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi kwa Taifa.
Mradi huo kutoka Dar es salaam hadi Morogro umekamilika kwa asilimia 100, na Morogoro hadi Dodoma asilimia 99, mradi umebakiza asilimia moja ili kukamilika kutoka Dar es salaam-Dodoma