Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha muswada wa sheria ya ongezeko la kodi kwa watalii kutoka nje ya Tanzania wanaokuja kutembelea hifadhi.
Baada ya muswada huo kupita bungeni baadhi ya mawakala wa utalii jijini Arusha walitoa taarifa kwenye chama chao kwamba zaidi ya wageni 2000 wamekatiza safari kutokana na ongezeko hilo na wakasema serikali itapoteza zaidi ya bilioni 1.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ‘TANAPA’, Allan Kijazi amepata nafasi ya kulizungumzia hilo na kusema……
>>>Wengi wamekuwa wakilalamika lakini kama mnavyofahamu kodi yenyewe ya VAT imeanza July 01 na leo ni siku ya tatu tu, kwa hiyo hatuna takwimu za kutosha kuonyesha kuwa wageni watapungua au wamepungua kutokanana ongezeko hilo.
>>>Kwa hiyo nadhani baada ya mwezi mmoja au miwili ndio tunaweza tukawa na takwimu ambazo tunaweza kuzionyesha kitaalamu kuonyesha kuwa wageni wamepungua, sasa hivi ni malalamiko, tunachulia kwamba ni malalamiko lakini bado hakuna takwimu sahihi kwamba mabadiliko hayo yana ukweli au ni hofu tu imejengeka:- Allan Kijazi
Aidha Katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi amefungua ofisi za ‘TANAPA’ kwa mkoa wa Dar es salaam ambayo itasaidia kwa wakazi wa Dar es salaam kutatuliwa kero zao kwa haraka zaidi ikilinganishwa na hapo awali ambapo iliwaladhimu kwenda kwenye mikoa kama Arusha kwa ajili ya huduma.
ULIKOSA HII YA WATALII KUSITISHA SAFARI YA KUJA TANZANIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI