Baba mzazi wa winga wa Barcelona na Uhispania Lamine Yamal yuko hospitali baada ya kuchomwa kisu usiku wa kuamkia jana.
Mounir Nasraoui, 35, alipata majeraha mengi ya kuchomwa kisu wakati wa ugomvi mwendo wa saa tisa alasiri katika wilaya ya Rocafonda ya Mataro, mji ulio kaskazini-mashariki mwa Barcelona.
Nasraoui alikimbizwa katika Hospitali ya Can Ruti ambapo utambuzi wake wa awali ulisemekana kuwa mbaya lakiini usiku wa manane, hali ya Nasraoui iliripotiwa tena kuwa thabiti.
Mapema Jumatano, maafisa wa polisi walilazimika kuingilia kati huku watu watatu wakimzonga na kumrushia maji Nasraoui alipokuwa akitembea barabarani na mbwa wake.
Katika video iliyorekodiwa na mtu kutoka ghorofa karibu na eneo la tukio, Nasraoui alionekana akiongozwa na mwanamume kabla ya kuzungumza na maafisa wawili wa polisi.
Saa 11.30 jioni Jumatano jioni, Mossos d’Esquadra ilithibitisha tukio hilo la kuchomwa kisu kwa mwanaume huyo na kusema watu watatu wamekamatwa.
Nasraoui alibaki hospitalini mapema Alhamisi asubuhi akiandamana na ndugu, ambaye inasemekana alikuwa akiwasiliana mara kwa mara na Yamal.
Wawakilishi wa winga huyo wa Barcelona pia walisafiri kwenda hospitalini, huku familia ikipokea uungwaji mkono kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo.