Huko Missouri Marekani Wateja 140 waliokwenda kutengeneza nywele saluni wamekutwa hawana virusi vya corona licha ya kuhudumiwa na Wahudumu wawili wa saluni hiyo ambao walikua na corona.
Wafanyakazi hao wawili wote walifanya kazi wakiwa na corona kwa zaidi ya wiki bila kujijua lakini uzuri ni kwamba saluni hiyo ilifata maelekezo ya Wataalamu wa Afya ikiwemo Wafanyakazi hao kujifunika nyuso zao na viti kuwekwa mbalimbali.
“Hii ni habari nzuri sana kuhusu umuhimu wa kuvaa barakoa, utafiti unaonesha njia mbili kuu za kuepuka corona ni kuvaa mask na kukaa mbalimbali” – Idara ya Afya Missouri
“Mmoja wa Wafanyakazi hao alihudumia Wateja 56 na mwingine 84, Wateja wetu wote hao waliopimwa corona hawajakutwa nayo, Wafanyakazi wanaendelea vizuri” – Uongozi wa Saluni hiyo umesema.
Zaidi ya Watu laki moja na elfu 12 wamefariki kwa corona nchini Marekani huku idadi ya Wagonjwa ikizidi milioni 2, kwa Missouri tu wamefariki Watu 850 na Wagonjwa zaidi ya elfu 15.