Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe. Christopher Ngubiagai amewatala Maafisa Tarafa na Watendajo wa Kata kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi ya mfumo wa Force Account ili kuondoa hoja za ukaguzi katika ngazi ya msingi.
Mhe. Ngubiagai ametoa kauli hiyo tarehe 29 Aprili, 2024 wakati akifunga mafunzo kwa Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza jijini Mwanza.
Mhe. Ngubiabai amesema Mfumo wa ‘Force Account’ unahusisha matumizi ya fedha kidogo kwa matokeo makubwa hususani katika kutekeleza miradi ya maendeleo, kutumia mafundi wa kawaida (Local Fundi) pamoja na kuwasimamia kwa kutumia wataalam wa ndani, ni mfumo mzuri ila msipousimamia kukamilifu hautaleta tija na tutaishia kupata hoja.
Mhe. Ngubiabai ameongeza kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinapelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma za msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya, shule, zahanati na miundombinu mingine lakini ngazi hizo hakuna wataalam wa kufanya manunuzi, Wahasibu na Wahandisi hivyo nyie ndio mnapaswa kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa ili kuondoa hoja za ukaguzi na kudhibiri upotevu wa fedha za Serikali.
“utaratibu huu wa ‘force account’ umeonyesha manufaa makubwa kwa kutumia fedha kidogo kwa kazi kubwa, yapo maeneo yaliyofanya vizuri sana kupitia utaratibu huo lakini pia yapo maeneo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa unaotokana na usimamizi hafifu na kupelekea miradi kukamilika chini ya viwango hivyo thamank ya fedha kukosekana hivyo mfumo wa ‘force account’ ila ongezeni usimamizi’ alisema Mhe. Ngubiagai. Aidha, ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kuangalia uwezekano wa kuwapatia fedha za uendeshaji wa ofisi za Tarafa na Kata ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.