Rais wa Kenya William Ruto ametangaza kuwa mitandao miwili ya kijamii imekubali kuwalipa watengeneza maudhui( content creators) kutokana na maudhui wanayotengeneza nchini humo kufuatia mazungumzo ambayo amefanya na vuongozi wa mitandao hiyo.
Ruto aesema hayo ikulu jana wakati wa kuzindua tamasha la muziki la Kenya ambapo miongoni mwa kampuni hizo ni Facebook ambayo imekubali kufanya majaribio kwa content creators 25 wa Kenya ili kuona jinsi maudhui yao yanaweza kutengeneza mapato.
Katika kipindi cha mwaka mmoja nimejadiliana na wamiliki wa mitandao ya kijamii kuanzia Facebook, Tweeter, TikTok, hadi Youtube na tukaendeleza mazungumzo yetu, amesema Ruto.
Kauli ya Ruto inakuja wiki chache baada ya Elon Musik kuanza kuwalipa watumiaji wa mtandao wa X zamani Tweeter kutokana na maudhui yao ikiwemo posts za kawaida na video na kupokea sehemu ya mapato yanayotokana na matangazo ambapo waliolipwa ni wenye akaunti ambazo zimejisajili kwenye Tweeter Blue(X Premium) pekee na zenye views Zaidi ya milioni 5 kwa kila chapisho.