March 15 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na waajiri wote kwa ujumla kuchukua hatua ya kuhakikisha katika Taasisi zao hakuna watumishi hewa na ajira batili ifikapo March 30 2016.
April 05 2016 ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imezidi kulifuatilia kwa ukaribu agizo hilo la Rais ambapo imetoa taarifa ambapo Waziri Angellah Kairuki ameyazungumza haya…..
>>>’kwa mujibu wa taarifa ya awali zilizowasilishwa na wakuu wa mikoa mbalimbali walibainisha watumishi 1,830 kama watumishi hewa. Aidha kwa mujibu wa taarifa hizo dosari iliyobainika ni kukosa majina ya watumishi hao hewa na walioondolewa katika mfumo kwa sababu nyingine mbalimbali kama utambulisho wa watumishi’:-Angellah Kairuki
>>>’Ofisi yangu imewaagiza waajiri wote wawe wamewasilisha taarifa zao wiki hii ili kutuwezesha kujua kwa usahihi watumishi wangapi ni hewa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa’:-Angellah Kairuki
UNAWEZA KUJIONEA IDADI YA WATUMISHI HEWA WALIOONDOLEWA KATIKA MFUMO KUANZIA JANUARY 01 HADI APRIL 05 2016.
ULIIKOSA VIDEO YA RAIS MAGUFULI KUTOA MASAA 360 KWA WANAOLIPWA MISHAHARA FEKI? ANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI..
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line yatiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE