Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa takwimu za vifo vinavyotokana na uvutaji wa sigara ambapo mwaka 2017 watu Milioni 8 walifariki kutokana na uvutaji wa sigara
Mbali na takwimu hizo, hadi sasa watu Milioni 16 wanaoishi Marekani wamebainika kuwa na magonjwa yanayohusisha na uvutaji sigara.
Mwaka 1988 Shirika la Afya Duniani liliazimia kuifanya May 31 kila mwaka kuwa siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani ikiwa ni moja ya namna ya kupunguza vifo vinavyotokana na uvutaji
Nchi za Kipato cha chini na cha kati zimeripotiwa kuwa na watu wengi wanaotumia sigara duniani katika jumla ya watu Bilioni 1.3 wanaotumia tumbaku
Vifo Millioni 100 vimeripotiwa kutokana na uvutaji wa sigara kwa Karne ya 20. Aidha Katika wavutaji 1.3 Bilioni watu Milioni 7 hufa kutokana na madhara ya moja kwa moja ya uvutaji.
Watu Milioni 1.2 katika wavutaji Bilioni 1.3 wameripotiwa kufariki kutokana na madhara yasiyo ya moja kwa moja ya sigara na tumbaku.