Katibu tawala Mkoa wa Dar es salaam Rehema Madenge amewataka watoa huduma za afya Mkoani humo Kujiepusha na Lugha zisizo na Staha Kwa wagonjwa badala yake wajielekeze Kuboresha huduma Kwa wateja na kusimamia maadili ya kazi zao
Madenge ametoa kauli hiyo wakati wa kikao na Waganga wafawidhi wa vituo vyote vya umma Mkoa wa Dar es salaam pamoja na wasimamizi wa eneo Hilo kutoka ngazi za Halmashauri Mkoa na Hospitali wa rufaa za mikoa Mwananyamala,Amana na Temeke Kwa lengo la kutathmini Hali ya utoaji wa huduma za afya ili kuweka mipango thabiti ya kuhakikisha huduma zinaboreshwa zaidi.
Aidha ametumia nafasi hiyo kusema kuwa suala la kujitathimini katika utoai wa huduma za afya ni Muhimu ili kuweka mipango ya Kuboresha maeneo ambao yanakabiliwa na changamoto.
Hata hivyo Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es salaam Dkt Rashid Mfaume amesema huduma Kwa ateja katika maeneo ya kutolea huduma za afya imeimarika na kwamba wataendelea kufuatilia iwapo kama kuna baadhi ambao hawazingatii maadili ya taaluma hiyo.
Katika kikao hicho imeshuhudiwa Halmashauri na vituo vya kutolea huduma za afya vilivyofanya vizuri vikitunukiwa vyeti na tuzo kama sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wao katika kutoa na kusimamia huduma Bora za afya.