Watoto wawili walikosa makazi Husna Bakari Abdallah na Ernest Michael Mbwambo wamejengewa nyumba na kanisa la pentekoste umoja lililoko Hedaru wilayani same mkoani Kilimanjaro ,zilizo ghalimu jumla ya shilingi milioni kumi na tatu laki mbili na elfu kumi.
Akisoma tarifa kwa Mgeni rasmi Mratibu wa kituo cha maendeleo ya mtoto na kijana cha pentekoste umoja ,ndugu Martin Eliaza Fiken amesema kituo hicho kinajishuguli mbalimbali zinazomhusu mtoto na kijana hasa katikakuwalinda na kuwalinda dhidi ya vitendo viovu kama vile ukatili.
“ndugu mgeni rasmi tunakukaribisha katika ufunguzi wa nyumba mbili za walengwa ambazo kanisa limewajengea Watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.Nyumba hizo zimegharimu shilingi milioni kumi na tatu laki mbili na elfu kumi tu,ambapo kanisa limeshirikiana na shirika la compassion international Tanzania kuwajengwa Watoto hawa”Amesema Martin
Aidha Ameongeza kuwa kanisa na Compassion kama mawakili wa watoto wanatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia tamko la kumlinda mtoto dhidi ya matukio ya kiunyanysaji.
Naye askofu wa kanisa hilo la pentekoste Umoja Godfrey Mhando amesema anashukuru shirika la Compassion kwa kukubaliana na kukaa pamaoja na kanisa kuwasaidia Watoto hawo ambao ni wahitaji kwenye jamii ya watu wa hedaru.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Same afisa tarafa ya Chome/Suji ndugu Sixbert Sarmeti amewataka wazazi,walezi na mashirika binafsi kuendelea kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili ili waweze kutimiza ndoto zao.
“ukatili upo kila sehemu sisi kama serikali na wadau mbalimbali tumeendelea kutoa elimu kwa jamii na sasa ukatili unaanza kupungua, hivyo niwaombe wazazi ,walezi na ndugu zetu hawa wa kanisa na pia mashirika binafsi kuendela kushirikiana na kuhakikisha mtoto huyu tunamlinda na mwisho wa siku aweze kutimiza ndoto zake”amesema Sixmas.
Mmoja wa wazazi wa Watoto hao waliopatiwa nyumba hizo Regina Yonas amelishukuru kanisa na kusema kuwa watatunza na kulinda nyumba hizo