Takriban watoto 447 na wanawake 248 ni miongoni mwa 1,417 waliouawa katika mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza, wizara ya afya ya Palestina ilisema Alhamisi.
Wizara pia imeripoti majeruhi 6,268 tangu Jumamosi.
Mapema siku ya Jumamosi, mkurugenzi wa hospitali ya al-Shifa katika ukanda huo aliiambia Al Arabiya kwamba zaidi ya asilimia 50 ya waliouawa na mashambulizi ya Israel kwenye ukanda huo ni wanawake na watoto.
“Mfumo wa huduma za afya huko Gaza umeporomoka,” alisema, akiongeza kuwa hospitali haiwezi tena kupokea watu wengine waliojeruhiwa.
Pia alionya kuwa kukatika kwa umeme kutasababisha vifo vya watu kadhaa na kutoa wito wa kufunguliwa kwa njia salama za kupeleka vifaa vya matibabu.