Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekadiria kuwa hadi siku hii ya kwanza ya mwaka itakapoisha, kuanzia Fiji, ambako mwaka mpya uliingia mapema hadi kule Marekani ambako wao waliuona mwaka kwa kuchelewa, kutakuwa na watoto zaidi ya 371,504 walizaliwa kote ulimwenguni.
Kupitia uchambuzi wa sensa ya kitaifa na data ya usajili na pia ripoti ya Umoja wa Mataifa Mtazamo wa Idadi ya Watu, UNICEF inakadiria kuwa jumla ya takriban watoto Milioni 140 watazaliwa ulimwenguni mwaka 2021, wakiwa na wastani wa umri wa kuishi wa miaka 84.
Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Fowler “watoto waliozaliwa Siku ya Mwaka Mpya wamekuja kwenye ulimwengu tofauti kabisa na mwaka mmoja uliopita” kwa mustakabali wa watoto hawa, ametaka jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja akisema, “ufanye mwaka 2021 uwe aina ya Mwaka wa haki zaidi, salama na afya kwa watoto.”
Fowler ameongeza “wakati ulimwengu unakabiliwa na janga jipya la corona, kushuka kwa uchumi, kuongezeka kwa umaskini na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kazi ya UNICEF ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.
KAMATA KAMATA BIASHARA HARAMU WANAOHIFADHI WALEMAVU ILI WAKAOMBE MTAANI