Serikali imeendelea na juhudi za kupambana kuurejesha Mji wa Kateshi katika hali yake ya kawaida kama ilivyokuwa awali baada ya Mafuriko yenye tope na Magogo ya mti kuharibu makazi ya watu pamoja na kugharimu maisha ya Watanzania zaidi ya 80.
Katika tukio hili waathirika wa Mafuriko haya wamepatiwa hifadhi na Serikali,lakini bado Wadau mbalimbali wakiwemo likiwemo Shirika la kimataifa la Save The Children limetoa vifaa kwaajili ya watoto kwaajili ya Michezo kwa lengo la kuwatoa mawazo juu ya tukio hilo ambapo vifaa hivyo ni zaidi ya shilingi Milioni 30
Shirika hilo limekuwa likitoa misaada mbalimbali nje ya Msaada huo kwaajili ya watoto lengo ikiwa ni kuwapa faraja waathirika wa Mafuriko pamoja na kuunga mkono juhudi na Jitihada za Serikali ya awamu ya sita.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Serikali Mkuu wa wilaya ya Hanang Janeth Mayanja amesema msaada huo ndio wa kwanza katika Kulenga kundi la watoto hasa katika michezo huku akiamini kwamba itachangia kurejesha furaha kwa watoto hao.