Mamlaka za Niger zimesema takriban watu 100 wameuawa na Wanamgambo huku wengine 75 wakiachwa na majeraha baada ya mashambulizi kutokea katika Vijiji vya Tchombangou na Zaroum-dareye kwa wakati mmoja.
Waliofanya mashambulizi walitumia pikipiki, walijigawa katika makundi na kuyatekeleza kwa wakati mmoja katika maeneo hayo yaliyopo upande unaopakana na Mali ambapo inasemekana mashambulizi yametokea kufuatia madai kuwa, Wanakijiji wameua Wanamgambo wawili.
Niger inakabiliwa na mapigano ya kijamii na kutoka kwa makundi mbalimbali, lakini hadi sasa hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo.