Jeshi la polisi kushirikiana na TCRA na Benki ya Tanzania wamefanikiwa kuwakamata Watu 12 kwa tuhuma za kujihusiha na utapeli Kwa njia ya mtandao kupitia kampuni ya inayofahamika kwa jina la LEO BENETH LONDON maaruku kama LBL .
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro SACP .ALex Mkama amesema Watu hao wamekamatwa wakiwashawishi Watu kujiunga na kampuni hiyo inayoendesha biashara hiyo mtandaoni bila ya kuwa na kibali kutoka Benki Kuu jambo ambalo ni kosa kisheria.
Rpc Mkama amesema baadhi Yao wamekutwa na vijana zaidi ya mia.moja wakiwa wamewafungia ndani na kuwapa elimu namna ya kufanya baishara hiyo kwa.madai ya kuwapa ajira.
Amesema biashara hiyo inachezwa mtandaoni ambapo Watu wanatakiwa kutazama video fupi ndipo wapate fedha ambapo wanatakiwa kutoa kiingilia kuanzia shilingi elfu hamsini (50000) ,laki moja na hamsini (150000) na Shilingi laki Tano na arobaini (540,000).
Amesema baadhi ya watuhumiwa wamekutwa tayari wamechukua fedha milioni 20 ambazo tayari zipo mtandaoni na kuwaahidi kuwa watakuwa mabilionea.
Amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.