Watu wasiopungua 20 wanaripotiwa kufariki dunia nchini Bangladesh na makumi ya wengine kujeruhiiwa kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo ya bara Asia.
Mamlaka husika nchini humo zimetrhitibisha kwamba, kwa akali watu 20 wameaga dunia na wengine zaidi ya milioni 5.2 wameathiriwa na mafuriko yaliyosababisha na mvua kubwa na mito iliyojaa maji kupita kiasi nchini Bangladesh.
Mafuriko hayo yamesababisha kutokea janga la kibinadamu na kuwaacha raia nchini humo wakihitaji misaada ya haraka nay a dharura ya chakula, maji safi, dawa na nguo kavu, hasa katika maeneo ya mbali ambako barabara zilizofungwa zimekwamisha juhudi za uokoaji na misaada.
Mshauri mkuu wa serikali chini ya uongozi wa Mohammad Yunus ameziambia duru za habari kkwamba, serikali imechukua hatua zote zinazohitajika kuhakikisha hali ya kawaida inarejea kwa wahanga walioathiriwa na janga hilo la kimaumbile.
Zaidi ya watu 400,000 wamehifadhiwa katika vituo 3,500 vilivyotengwa kuhudumia wahanga wa mafuriko katika wilaya 11 zilizoathirika na mafuriko hayo nchini Banglad