Karibia watu 22 wamethibitishwa kufariki baada ya boti la watali kuzama katika jimbo la Kerala kusini mwa India wengi wao wakihofiwa kuwa watoto.
Hadi tukichapisha taarifa hii haikuwa imebainika ni kwa nini boti hiyo iliyokuwa imewabeba karibia watu 30 kuzama siku ya Jumapili katika wilaya ya Malappuram kusini mwa jimbo la Kerala
Shughuli ya kutwatafuta manusura wa ajali hiyo ya boti imekuwa ikiendelea tangu siku ya Jumapili kujaribu kuwatafuta watu ambao huenda wanahofiwa kuwa huenda wamezama.
Kutokana na picha ambazo zimenaswa kutoka katika eneo la tukio, raia wa kujitolea wameonekana wakitumia Kamba kujaribu kuzuia boti hilo kuzama zaidi, wengine wakionekana wakichungulia kwenye madirisha kubaini iwapo kuna manusura.
Mamlaka inayohusika na shughuli ya uokozi imesema kwamba wamepata miili 22, kati ya hizo, 15 ni za wanawake na nyengine 15 ikiwa ya wanaume.