Watu wanne wameuawa katika shambulio la Jumapili kwenye madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh ya Washia nchini Iran, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.
“Takriban watu wanne waliuawa kufuatia shambulio la kigaidi lililotekelezwa na watu wawili wenye silaha dhidi ya madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh” huko Shiraz, mji ulio kusini mwa Tehran, kulingana na shirika rasmi la habari la Irna. Mmoja wa washambuliaji alikamatwa huku mwingine akiwa bado hajakamatwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim.
Mmoja wa washambuliaji amekamatwa, huku mwingine akiwa bado hajakamatwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim.
Shah-Cheragh, eneo muhimu sana la mahujaji wa Kishia nchini Iran, lililengwa na shambulio lililosababisha vifo vya watu 13 mnamo Oktoba 26, 2022.
Wanaume wawili waliohusika katika shambulio hili lililodaiwa na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS) walinyongwa hadharani huko Shiraz mnamo Julai 8.
Watu hao wawili walipatikana na hatia ya “ufisadi katika ardhi ya Iran, uasi wa kutumia silaha na kuhatarisha usalama wa taifa”, pamoja na “njama dhidi ya usalama wa nchi”. Pia walishtakiwa kwa kuwa uhusiano na kundi la Islamic State na “njama dhidi ya usalama wa nchi”.