Watu wanne waliuawa na wengine watano kujeruhiwa huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa leo asubuhi, wizara ya afya ya Palestina imesema.
Haya yanajiri baada ya vyombo vya habari vya Israel kuripoti makabiliano makali ya kurushiana risasi kati ya wanajeshi wa Israel na Wapalestina katika eneo hilo katika vita vilivyojumuisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.
Ghasia zimeongezeka katika Ukingo wa Magharibi tangu vita kati ya Israel na Gaza kuzuka.
Tangu wakati huo, Wapalestina 115, wakiwemo watoto 33, wameuawa, kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu (OCHA).
Nusu ya waliofariki ni wakati wa mapigano yaliyofuatia operesheni za kuwasaka na kuwakamata Israel, ilisema.