Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lemesema jumla ya watu 557 wamefariki dunia na 891 wamejeruhiwa kutokana na matukio ya moto, maokozi na ajali za barabarani, mafuriko kwenye migodi, mashimo ya vyoo, mito, mabwawa, baharini na maeneo mengine katika kipindi cha Januari 2020 mpaka Desemba 30, 2020.
Pia limesema limekabiliana na matukio ya Moto yapatayo 1925 huku matukio ya maokozi yakiwa 845.
Mkaguzi wa Jeshi hilo, Joseph Mwasabeja, ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio waliyokabiliana nayo kuanzia Januari 2020 Hadi Desemba, 2020.