Polisi wa Afrika Kusini walisema Jumanne kuwa wamewakamata watu sita kwa mauaji ya mwaka jana ya mmoja wa wasanii wa rap nchini humo, Kiernan Forbes, anayejulikana kama AKA.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 10 mwaka jana alipokuwa akitembea na rafiki yake nje ya mgahawa maarufu wa Durban saa chache kabla ya kutumbuiza katika klabu iliyo karibu.
“Watu sita wamekamatwa ambao watafikishwa mahakamani siku ya Alhamisi” waziri wa polisi Bheki Cele aliambia mkutano na waandishi wa habari mjini Durban.
Alisema mshukiwa mkubwa alikuwa na umri wa miaka 36 na kwamba wengine wanaweza kuongezwa kwenye orodha hiyo.
Kamishna wa polisi wa mkoa huo Nhlanhla Mkhwanazi aliwaambia waandishi wa habari kwamba “bwana akili”, watu wawili wenye bunduki, waangalizi wawili na “mratibu wa silaha na magari” wote wako chini ya ulinzi.
Watu kadhaa ya waliokamatwa walihusishwa na kesi za mauaji ya kutisha, alisema, na wawili walikuwa wameshikiliwa katika nchi jirani isiyo na bandari ya Eswatini.