Watu 80 wanashikiliwa na Polisi Nchini China kwa kutengeneza dawa inayofanana na Chanjo ya Corona Virus kwa kuweka maji yenye chumvichumvi tu.
Hadi sasa katika Jimbo la Jiangsu na Shandong chanjo feki zaidi ya 3,000 zimekamatwa. Polisi hawajaweza kusema ni chanjo kiasi gani zimeuzwa.
Sinopharm ni chanjo ambayo ilithibitishwa kutumika China mwezi Desemba ili kuwalinda Wananchi takriban milioni 50 wa China.