Serikali ya Kenya inawatafuta watu 85 ambao walichangamana na mwanamke aliyethibitika kuwa na Corona virus. Mgonjwa huyo wa COVID 19 alitoroka Hospitali ya Mbagathi, alipokuwa ametengwa kusubiri majibu.
Alifuatiliwa na akarudishwa na Maafisa wa Usalama. Hakutaja ni wapi alienda baada ya kutoka Hospitalini. Shirika la Afya Duniani, limesema Nchi nyingi zilizo na kesi zilizothibitishwa huwa na ongezeko kubwa la maambukizi.
Kenya ilithibitisha mgonjwa wa kwanza wa corona virus Ijumaa iliyopita, hadi sasa Kenya imethibitisha watu 7 kuwa na Corona Virus.