Takriban watu 100 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi na mafuriko katika Mji wa Petrópolis nchini Brazil.
Jiji hilo, ambalo liko kwenye milima kaskazini mwa Rio de Janeiro, lilikumbwa na mvua kubwa.
Nyumba katika vitongoji vya milimani ziliharibiwa na magari kusombwa na maji huku mafuriko yakipita katika mitaa ya jiji hilo.
Timu za utafutaji na uokoaji zinakabiliana na tope kutafuta walionusurika.
Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Brazil lilisema kwenye Twitter watu 24 wameokolewa wakiwa hai hadi sasa, na vifo 94 vilivyothibitishwa.