Shirika la msalaba mwekundu nchini Libya, limesema idadi ya watu waliofariki katika mafuriko kwenye mji wa Derna imefikia watu elfu kumi na mmoja.
Idadi hii pia inatarajiwa kuongezeka wakati huu shughuli za kutafuta miili zaidi iliyokwama kwenye udongo ikiendelea.
Mamlaka nchini humo imeeleza kuwa karibia raia elfu 30 wamepoteza makazi yao, wakati huu pia wanasiasa kwenye taifa hilo wakitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi katika mafuriko hayo mabaya zaidi.
Idadi kubwa ya raia wa Libya wamehusisha mkasa huo na hali mbaya ya miundombinu kwenye taifa hilo.
Umoja wa mataifa kwa upande wake umekashifu mifumo ya kutoa tahadhari kuhusu majanga nchini Libya.
Mkuu wa shirika la kutathmini hali ya anga amesema sehemu kubwa ya vifo vilivyoripotoiiwa nchini Libya vingeepukika iwapo raia wangetahadharishwa mapema na kupewa muda wa kuondoka.