Shirika la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Mataifa (OCHA) lilisema watu wasiopungua milioni 7.1 wana uwezekano wa kukumbwa na ukosefu mkubwa wa chakula nchini Sudan Kusini kati ya Aprili na Julai.
Ripoti mpya iliyotolewa Jumapili jioni na OCHA ilisema hadi tarehe 30 Aprili, mgogoro wa Sudan umesababisha watu 655,694 waondoke nchini humo na kwenda Sudan Kusini, ambapo kwa wastani watu takriban 1,800 wanaingia Sudan Kusini kila siku.
Kwa mujibu wa OCHA, watu elfu 79 wako katika hali ya maafa, ambapo wengi wao wanaishi katika maeneo yanayokabiliwa na athari ya tabianchi, kuyumba kwa uchumi, au mapambano.