Leo September 10, 2020 Watu nane wamekutwa wakiwa wameuawa katika Hifadhi ya Isawima iliyopo Wilaya ya Kaliua mkoani humo, chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana hadi sasa.
Watatu kati yao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 25-40 huku watano wakiwa Watoto wenye umri wa miaka miwili hadi kumi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi Barnabas Mwakalukwa amethibitisha tukio hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na amesema tukio hilo limetokea Septemba 6,2020.