Mkoani Njombe watu wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika wilaya ya kipolisi mjini Makambako kwa tuhuma za kukutwa na nyaya za umeme zenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 43 zinazotumika kusambazia umeme wa mradi wa REA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema hatua hiyo imekuja baada ya Polisi kufanya upelelezi na kuwanasa watuhumiwa hao, kufuatia aliyekuwa msimamizi wa mradi wa REA katika Kata ya Kichiwa Tarafa ya Makambako kutoa taarifa kwenye Jeshi hilo alipogundua dram sita za nyaya za umeme zenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 43 zimeibiwa.
“Tumekamata gari aina ya fuso na imebeba waya Rol zipatazo sita na hizi rol zipo nyaya za aina mbili tofauti zinazotumika kwenye umeme wa rea hapa mkoani Njombe” RPC Hamis Issa
“Tuliweza kubaini kutokana na nyaraka iliyodondoka ya faini iliyotozwa hii gari,ikajulikana iko Dar Es Salaam,amefuatwa tajiri akasema gari iko Katavi na tulipofuatilia tuliikuta Mlele sehemu moja inatwa maji moto” RPC Hamis Issa
“TUNAANZA KUGOMBANA, CCM MSIPENDELEE” MAALIM SEIF AGEUKA MBOGO MBELE YA MA-RC, DC