Umoja wa Mataifa unasema watu wengine milioni moja kuikimbia nchi watu wengine milioni moja kuikimbia nchi hiyo, huku mkuu wa majeshi akitowa wito kwa vijana kujiunga na vita.
Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa jioni ya Jumanne (Juni 26) ilisema licha ya ghasia hizo kuelekezwa kwa kiasi kikubwa kwenye mji mkuu, Khartoum, ambako jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah Burhan na wanamgambo wanaoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo wanawania udhibiti, mauaji makubwa yanashuhudiwa pia jimbo la magharibi la Darfur, ambako wanamgambo wa Dagalo na washirika wao wa Kiarabu wanawaandama raia wa makabila mengine yasiyo ya Kiarabu.
Umoja wa Mataifa ulionya kwamba mzozo nchini Sudan unaweza kuwalazimisha watu 800,000 kuikimbia nchi hiyo huku mapigano kati ya makundi hasimu ya kijeshi yakiendelea katika mji mkuu licha ya kudaiwa kusitisha mapigano.
Mamia ya watu wameuawa na maelfu kujeruhiwa katika mapigano ya siku 16 tangu mzozo kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kuzuka katika mzozo Aprili 15.
Hii leo jeshi la RSF nchini Sudan lilitangaza kuwa itawaachilia wafungwa 100 wa vita ikiwa ni sehemu ya sherehe za Siku kuu ya Eid, huku upande wa upinzani wa serikali ukitangaza kuwa hakutakuwa na mapigano leo.
Leo asubuhi Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitangaza likizo ya siku moja ya kusherehekea Eid al-Adha.
Hii ni moja ya siku muhimu zaidi katika kalenda ya Kiislamu ya ulimwengu.
Taarifa iliyotumwa kwenye akaunti ya Facebook ya serikali ya Sudan inasema kwamba “siku hii ya Eid, jeshi linatangaza kusitisha mapigano katika siku ya kwanza ya Eid al-Adha.”
RSF mnamo Jumanne pia ilitangaza kwenye Facebook kwamba kutokana na likizo ya Eid al-Adha, itawaachilia wafungwa 100 wa vita siku ya Jumatano.
Taarifa ya RSF inasema kwamba walioachiliwa “walinaswa na mamlaka zao na kutumwa kupigana vita ambavyo havikuwa vyao”.