Watu wenye silaha waliwateka nyara watu 40 kutoka kanisani katika kijiji cha mbali kaskazini mwa Nigeria, kikundi cha Kikristo cha eneo hilo kilisema Jumatatu, katika shambulio la hivi karibuni dhidi ya waumini.
Shambulio hilo ni utekaji wa hivi karibuni wa watu wengi nchini Nigeria, ambako ukosefu wa usalama ni moja ya changamoto kubwa zinazomkabili rais mpya Bola Tinubu, ambaye atachukua hatamu za uongozi mwishoni mwa mwezi huu.
Washambuliaji Jumapili walivamia kanisa la Kibatista la Bege katika eneo la Chikun katika jimbo la Kaduna, awali wakiwateka nyara watu 40, ingawa 15 walifanikiwa kutoroka baadaye, mchungaji Joseph Hayab, mkuu wa chama cha Wakristo wa Nigeria katika jimbo la Kaduna, ameiambia AFP.
Msemaji wa polisi wa Kaduna amethibitisha shambulio la Jumapili lakini hakuweza kutoa maelezo zaidi.
Magenge ya wahalifu wenye silaha nzito wanaojulikana kama majambazi mara kwa mara huwateka nyara watu wengi kaskazini magharibi na katikati mwa Nigeria ili kulipwa fidia, na kuwashikilia mateka wao katika kambi ambazo ziko mafichoni ndani ya misitu mikubwa inayopatikana katika eneo lote hilo.
TAZAM:KUTOKA SINGIDA ALIPOZIKWA MWANAFUNZI WA UDOM NUSURA, NDUGU NA HOSPITALI WAONGEA “HAKUWA NA MAJERAHA”