Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter na mmiliki Elon Musk alisema kampuni hiyo itaondoa alama za tiki za bluu kwa watumiaji ambao hawajalipia $8 kwa mwezi kwa ajili nafasi ya usajili ya Twitter Blue.
Kampuni hiyo kubwa ya mitandao ya kijamii ilianza kuondoa uthibitishaji wa tiki ya bluu uliokuwa ukitamaniwa kutoka kwa maelfu ya akaunti kuanzia siku ya Alhamisi hatua hiyo inajiri huku mmiliki wake Elon Musk akijaribu kubadilisha kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii ili kupata faida. Watumiaji wanaotaka kuhifadhi tiki za bluu za majina yao lazima walipe $84 kwa mwaka (£67) ili kujisajili kwenye Twitter Blue.
Mabadiliko yalipotokea, wengi waliothibitishwa hapo awali walienda kwenye kurasa ya Twitter kufanya utani kuhusu hilo, au kueleza hasara walizopata.
Sasa, Twitter hatimaye imeua alama za bluu kwa watumiaji wasiolipa, lakini sio zote, kwani baadhi ya watu mashuhuri bado wana alama ya kuangalia licha ya kutolipa kwao.
Mmiliki wa twitter Elon Musk, ambaye uwekezaji wake wa dola bilioni 44 katika jukwa hilo alibadilisha mfumo huo mwenyewe kwenye Twitter akikiri kuwa yeye binafsi analipia tiki za bluu za William Shatner, LeBron James, na Stephen King. Na akaunti zote tatu bado zina alama zao za tiki ya blue ,Musk hakufafanua zaidi kwa nini alichagua kulipia alama hizo, na haijulikani ikiwa ana mpango wa kulipia zaidi.
Mwezi uliopita, mmiliki na bilionea wa Twitter, Elon Musk, alitangaza kuwa kuanzia Aprili 1, watumiaji walioidhinishwa kwa alama za bluu wataondolewa kwenye huduma isipokuwa walipe ada ya usajili ya $8 sawa na Tsh18,784kwa mwezi kwa Twitter Blue. Kwa mashirika, ada ni $1,000 kwa mwezi ili kuongeza mapato kwenye kampuni hiyo.
Watu maarufu kama vile Papa Francis na msanii Beyonce wakiwa miongoni mwa walioathrika.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, Bill Gates na Kim Kardashian wakiwa miongoni mwa matumiaji wa mtandao huo wa twitter ambao wamepoteza beji zao.